Moja ya Majimbo Manne
Jimbo la Tambarare
Jimbo la Tambarare ni mojawapo ya Majimbo manne ya KKKT Dayosisi ya Pare, linalohudumu kwa sehemu kubwa maeneo ya tambarare ya Wilaya ya Same.
Idadi ya Sharika
Sharika 15 zinazohudumiwa na Jimbo.
Mgawanyo wa Kanda
Jimbo limegawanyika katika kanda 2.
Eneo la Huduma
Wilaya ya Same, ndani ya KKKT Dayosisi ya Pare.
Muundo wa Jimbo
Sharika za Jimbo la Tambarare
Kanda ya Mashariki
Kanda ya Magharibi
Sharika za Misioni
Kanani na Kizungo.
Udiakonia na Huduma za Kijamii
Huduma za Jimbo kando na Uinjilisti
- Msaada wa mavazi, chakula na gharama za matibabu kwa familia zenye mazingira hatarishi kupitia Sharika zake.
- Mfuko wa Diakonia wa Jimbo unaosaidia watumishi wa Jimbo wanapopata misiba au wagonjwa.
- Huduma kwa wafungwa katika Gereza la Wilaya ya Same, ikiwemo sabuni, ndala, dawa za meno, miswaki, pedi na mafuta.
- Huduma kwa watumishi wastaafu 34 (wajane 8, Wainjilisti 21 na wachungaji 5) kupitia Mfuko Maalum wa Wastaafu.
- Huduma kwa washokeri na wagonjwa kwa kuwatia moyo kwa Neno la Mungu, Sakramenti na misaada mbalimbali ya kibinadamu.
- Huduma ya Mtoto na Kijana katika Usharika wa Kanisa Kuu na Usharika wa Ruvu, kwa watoto wanaoishi mazingira hatarishi, ikiwemo msaada wa kiroho, kielimu, kiafya na kijamii.
Huduma za Elimu
Shule zinazoendeshwa na Sharika
Shule ya Msingi na Awali ya Mkomazi
Shule mpya iliyoanzishwa mwaka 2021 karibu na makao makuu ya Dayosisi. Ni shule ya mchepuo wa Kiingereza inayoendeshwa na Usharika wa Kanisa Kuu.
Shule ya Awali na Chekechea Muungano
Shule ya Kanisa inayoendeshwa na Usharika wa Ruvu.